Kocha mkuu wa Azam FC , Youssoph Dabo anaamini wana nafasi ya kupata matokeo mazuri mechi ya marudiano na kuvuka hadi hatua ya kwanza ya michuano ya Kombe la Shirikisho.
Dabo alisema wachezaji wake walicheza vyema na baadhi ya makosa likiwemo la kipa ndio yaliyowaharimu, lakini atayafanyia kazi kabla ya marudiano.
“Bado tuna nafasi ya kusawazisha makosa na kupata matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani. Tunaenda kuandaa timu upya na naamini tutafanya vizuri kwenye mechi ya marudiano na kusonga mbele zaidi,” alisema Dabo.
Azam inahitaji ushindi wa bao 1-0 kwenye mechi ya marudiano ili kusonga mbele kwani ina faida ya bao la ugenini.