Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam: Tuko kamili kuwavaa Coastal Union

Azam Vs Art Solar 7 Bangala, Dube kuikosa Coastal Union

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benchi la Ufundi la Azam FC limeweka wazi kuwa bado wachezaji wao wawili hawajarejea kwenye uimara hivyo watakosekana kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Coastal Union ambao unatarajiwa kupigwa leo Ijumaa (Oktoba 06) kwenye Dimba la CCM Mkwakwani, jijini Tanga.

Kocha wa Azam FC, Yusuph Dabo amesema kuwa, wachezaji wao muhimu bado hawajatengamaa lakini hawana hofu wataendelea kupambana.

“Yannick Bangala na Price Dube hawa ni wachezaji wetu muhimu lakini bado hawajawa imara kutokana na kusumbuliwa na majeraha lakini waliopo wamekamilisha maandalizi kwa ajili ya mechi ya leo.

Kikubwa mashabiki wasiwe na hofu wazidi kuwa pamoja nasi, tushikamane kwa pamoja tunaamini tutafanya vizuri mechi hiyo.”

Mchezo uliopita Azam FC ilipata suluhu ugenini dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live