Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam FC awaachia msala Mbombo, Diao

Mbombo Idris.jpeg Kocha Azam FC awaachia msala Mbombo, Diao

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema kukosekana kwa Prince Dube kunamrudisha mshambuliaji, Idris Mbombo kusaidiana na Alassane Diao.

Akizungumza na Mwanaspoti, Dabo amesema ni mapema sana kuzungumzia pengo la Dube kikosini kwake kwani tayari ameandaa kikosi imara ambacho tayari kina wachezaji kuanzia wawili kila eneo.

“Ni kweli taarifa ya kukosekana kwake imetuyfikia lakini haina maana kwamba imu haitaweza kucheza mechi tuna kikosi kipana ambacho kina wachezaji zaidi ya wawili kila eneo kuna Idris Mbombo, Diao atafanya kazi ya Dube,” amesema Dabo na kuongeza;

“Tunatambua umuhimu wa Dube kwenye mechi mbili alizocheza kwa dakika nyingi zaidi amekuwa na mchango mkubwa hilo halipingiki lakini muhimu ni kuwajenga waliopo ili waweze kufanya kitu kikubwa zaidi.”

“Pointi za mapema kabla ya mzunguko wa mwisho ndio ambazo zinatoa uhakika wa timu kumaliza msimu vizuri, hivyo hizi ndio nyakati nzuri kujitengenezea nafasi nzuri ya kupata nafasi nyingine kmataifa baada ya kupoteza nafasi hiyo mapema msimu huu,” amesema Dabo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: