Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam FC atoa neno, Bangala mh..!

Yousuf Dabo Kocha wa Azam FC, Yousuf Dabo

Tue, 8 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Azam FC Youssouf Dabo amesema ana matarajio makubwa ya ushindani katika michuano itakayoshiriki baada ya kujipima katika mechi za kirafiki, huku kiungo Yannick Bangala akiwa na hatihati ya kuukosa mechi ya Ngao ya Jamii.

Azam imeshatua Tanga kwa mechi za Ngao ya Jamii, juzi usiku iliifunga Bandari Kenya kwa mabao 2-0 na Dabo aliliambia Mwanaspoti, kikosi kipo tayari kushindana baada ya kujipima kwenye mechi nne za kirafiki ameona uwezo wa kila mchezaji na mapungufu.

“Kikosi kipo tayari nafurahishwa na namna wachezaji wanavyopambana baada ya ushindi wa jana (juzi), tunasafiri kwenda Tanga kwa mchezo dhidi ya Yanga,” alisema Dabo na kuongeza;

“Tunatambua ugumu tutakaokutana nao kwani kila timu imejiandaa na nilishuhudia fainali ya Kombe la Shirikisho la (ASFC) Tanga.

“Nafahamu ubora wao hivyo sina hofu yoyote nimeanzaa kikosi changu kazi iliyobaki ni kwao kutumia vizuri dakika 90 za mchezo ili kuweza kutinga hatua inayofuata hatimaye kucheza fainali na kurudi na taji nyumbani.”

BANGALA HATIHATI

Kiungo mpya wa Azam, Yanick Bangala aliyetua kikosini hapo akitokea Yanga akakosa mchezo wa kwanza baina ya timu hizo mbili baada ya kupata majeraha.

Licha ya Azam kutoweka wazi, lakini Mwanaspoti linajua kiungo huyo alipata maumivu madogo wakati wa mazoezi.

“Ili kumuweka fiti mchezaji huyo ni wazi hawatamtumia kwenye mchezo wa Jumatano dhidi ya Yanga kwani, alipata shida mazoezi na mchezo wa jana dhidi ya Bandari hakutumika kutokana na shida hiyo.” kilisema chanzo hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live