Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Azam FC aichimba Yanga mkwara

Kally Ongala 25.jpeg Kocha wa Azam FC, Kally Ongala

Sat, 24 Dec 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya Azam FC kutopata ushindi katika michezo yake miwili iliyopita kocha wa timu hiyo, Kally Ongala, amesema mechi yao dhidi ya Yanga itatoa mwanga wa mbio zao za ubingwa.

Timu hizo zinakutana Jumapili hii ya Sikukuu ya Krismasi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa huku ukitarajiwa kuleta ushindani mkali kutokana ubora wa vikosi vyote vya pande mbili.

Akizungumza Kally alisema wanategemea ushindani mkali kutokana na ubora wa wapinzani wao ingawa malengo yao makubwa ni kushinda ili kupunguza gepu la pointi baina yao.

“Tulitegemea pointi sita kwenye michezo yetu miwili iliyopita dhidi ya (Kagera Sugar) na Geita Gold lakini kama ambavyo uliona haikuwa rahisi kwetu hivyo tunajipanga tena upya.

“Ushindi pekee utatufanya kupunguza pengo dhidi ya washindani wetu hivyo tunaungalia mchezo huo na kuuchukulia kwa umakini mkubwa licha ya ushindani tunaokwenda kukabiliana nao,” alisema.

Kally aliongeza baada ya kumaliza michezo yao miwili ya Kanda ya Ziwa kikosi kilianza safari ya haraka kurudi jijini Dar es Salaam ili kuweka miili fiti na kuanza programu za mchezo huo.

Mchezo huo unaofahamika kwa ‘Mzizima Derby’ unazikutanisha timu hizo zikiwa na kumbukumbu ya kufungana mabao 2-2 kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza.

Chanzo: Mwanaspoti