KOCHA msaidizi wa klabu ya Azam, Vivier Bahati ameweka wazi kuwa miongoni mwa changamoto kubwa ambayo kikosi chao kinapitia kwa sasa, ni kuwepo kwa kundi kubwa la wachezaji muhimu ambao ni majeruhi.
Azam jana Jumapili walikuwa na kibarua cha mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Kagera Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam Kuelekea mchezo huo Azam iliwakosa nyota wao wanne muhimu ambao ni Mathias Kigonya na Idd Nado waliokuwa wagonjwa, huku Lusajo Mwaikenda pamoja na Ayoub Lyanga wao wakiwa ni majeruhi.
Kocha Bahati alisema: “Kama kikosi tunajua hatujawa na matokeo mazuri mwanzoni mwa msimu huu, hali ambayo imekuwa ikitupa presha kubwa, lakini hali hii ni wazi inachangiwa na changamoto kubwa ya majeruhi ya wachezaji muhimu tuliyonayo.
“Kwa mfano wakati tunajiandaa na mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar tuliwakosa Kigonya na Nado waliokuwa wagonjwa na pia Lusajo pamoja na Lyanga ambao ni majeruhi.”