Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Asec ambeba Pacome

Kocha ASEC X Pacome Kocha Asec ambeba Pacome

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati mjadala wa kutojulikana kwa Pacome Zouzoua nchini kwao ukiwa unapamba moto kwa mashabiki kushambuliana, kocha Mfaransa aliyempandisha kiungo huyo amecheka kwa dharau kisha akafafanua kila kitu.

Kocha wa Asec Mimosas, Jullien Chevalier amesema kama kuna mtu ametamka Pacome hajulikani Ivory Coast hayo ni mawazo yake na sio watu wanaofuatilia soka la nchi hiyo hapo ndani.

Chevalier amesema anaheshimu mawazo ya watu lakini hawezi kukubaliana na hoja kwamba kiungo huyo hajulikani wakati kuwa ndiye mchezaji bora wa ligi kuu nchini humo akiibeba Asec kwenye mashindano yote kabla ya kusajiliwa Yanga. Kocha huyo amesema hatua ya kiungo mshambuliaji huyo kujumuishwa kwenye kikosi cha taifa cha awali kuelekea fainali za Mataifa Afrika zinazofanyika nchini humo pia ni ishara ya ukubwa wa Pacome.

"Kama kuna mtu amesema hivyo labda hafuatilii mambo ya soka, sidhani kama amesema kitu sahihi juu ya Zouzoua kwa hapa Ivory Coast, watu wa hapa wanapenda soka sana angalia wanavyoumia na matokeo ya timu ya taifa, hao watu wanashindwaje kumjua mchezaji bora wa ligi hapa," amesema Chevalier na kuongeza;

"Zouzoua ni mchezaji aliyefanya vizuri sana msimu uliopita Kimataifa na hata hapa ndani alikuwa kwenye kiwango bora sana, hata akipita anatembea hapa hatafika safari yake bila kusumbuliwa na mashabiki wanaomfahamu.

"Nadhani alistahili kubaki timu ya taifa naona jinsi mashabiki hapa wanaumia na kikosi cha taifa hili (Ivory Coast) licha ya kuwa na wachezaji wakubwa wanaoncheza Ulaya huu ni wakati wachezaji wanaocheza ligi ya ndani na hata hapoa Adrika kupewa nafasi pia."

Katika Ligi Kuu Bara Pacome amefunga mabao manne na kuasiti mara moja, huku akiwa ni mmoja wa nyota wanaoibeba Yanga kwa sasa katika Ligi Kuu Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika ambako pia amefunga mabao matatu na kuwa mmoja wa vinara wa mabao katika hatua ya makundi hadi sasa.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro alinukuliwa na chombo kimoja kwenye mahojiano yake na Waziri wa Michezo wa Ivory Coast, Adje Silas na kumjulisha juu ya uwezo wa Pacome na kuelezwa kushangaa akihoji Pacome ndio nani, licha ya mchezo huo kuitwa kikosi cha awali ya wenyeji wa fainali za Afcon 2023.

Hata hivyo sio kitu cha ajabu kwa Waziri kushindwa kumjua kwa vile yeye sio kocha, lakini mjadala kwenye mitandao ya kijamii imekuwa mkubwa na mashabiki wa Simba na Yanga kuchekana.

Chanzo: Mwanaspoti