Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Al-Merreikh ahofia balaa la Yanga

Osama Nabieh Kocha Osama Nabieh wa Al-Merreikh.

Mon, 4 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Al Merreikh ya Sudan, Osama Nabieh ameweka wazi kuwa na mtihani mzito mbele ya Yanga kutokana na ubora wa Yanga wa sasa lakini pia na mfululizo wa michezo ya ligi wanaoipata tofauti na wao.

Akizungumza kuelekea mchezo wao unaofuata dhidi ya Yanga kocha huyo alisema kuwa “Tunatarajia kukutana na upinzani mgumu kutoka kwa Yanga kutokana na ubora wao mkubwa ambao wamekuwa wakiuonyesha katika michuano ya kimataifa katika siku za karibuni.

“Pili wenzetu wanapata faida kubwa ya kucheza michezo ya ligi kuu ambapo inawapa uwezo mkubwa wa kujijenga zaidi na kufahamu wapi kuna mapungufu na wapi kunatakiwa kufanyiwa maboresho.

“Malengo yetu ni kuona tunafika makundi kama msimu uliopita,sisi tunayo changamoto ya kukosa mechi nyingi lakini naamini tutnayo nafasi nzuri ya kufanya vyema dhidi yao na kutimiza malengo yetu,”alisema kocha huyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: