Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Al Ahly: Tunafahamu umuhimu wa mchezo huu

Marcel Koller.jpeg Marcel Koller.

Tue, 24 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Barani Afrika Al Ahly, Marcel Koller, amesema kuwa anajua umuhimu wa mdhezo wa leo dhidi ya Simba SC, hivyo amezungumza na wachezaji wake kuhakikisha wanatumia vizuri kila nafasi watakayoipata ili waweze kupata ushindi na kusonga mbele.

Miamba hiyo inakutana baadae leo Jumanne (Oktoba 24), katika mchezo wa Mkondo wa pili wa African Football League utakaopigwa mjini Cairo, Misri saa kumi na moja jioni.

Kocha Koller amesema: “Mchezo uliopita tulitengeneza nafasi kadhaa ambazo kama tungekuwa makini basi tulikuwa na uwezo wa kushinda mchezo lakini haikuwa hivyo.

“Sitaki kurudia makosa yale, nimefurahi kuona wachezaji ambao waliukosa mchezo uliopita wanarudi na kuongeza nguvu kwenye kikosi changu ili tuweze kutimiza lengo letu la kwenda hatua inayofuata.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live