Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha Afariki Baada ya Mchezaji Wake Kukosa Penati

Kocha Dihoko Kocha Afariki Baada ya Mchezaji Wake Kukosa Penati

Thu, 10 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA wa Timu ya Kingurunyembe yenye maskani yake mjini Morogoro Emanuel Peter Dihoko amefariki kwa mshtuko baada mchezaji wake kukosa penati wakati wa mechi ya kirafiki na Timu ya Moro Kids.

Akithibitisha kutokea tukio hilo mtoto wa marehemu Alphonce Peter Dihoko amesema siku ya tukio timu ya Kingurunyembe ambayo alikua akiifundisha ilikua ikicheza mechi ya kirafiki na Timu ya Moro Kids ambapo tayari alifungwa bao 2-1 hivyo baada ya kupata nafasi ya penati aliamini timu yake itasawazisha lakini mchezaji wake alikosa penati hiyo ndipo akaanguka ghalfa kwa mshituko.

Alipelekwa hospitali moja mjini humo kabla ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili ndipo umauti ukamkuta.

Marehemu Dihoko aliwahi kuchezea Timu mbalimbali za ligi kuu ikiwemo Sigara, Reli, Kagera na badae kugeukia ukocha na kufundisha Timu ya Dar City na hadi umauti inamkuta alikua anafundisha timu ya Kingurunyembe inayoshiriki ligi daraja la Tatu mkoani Morogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live