Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha ASEC aukubali muziki wa Simba SC

Simba 13 1536x1025 Kocha ASEC ainyooshea mikono Simba SC

Wed, 16 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

KOCHA Mkuu wa Asec Mimosas, Julien Chevalier raia wa Ufaransa, ameukubali muziki wa Simba na kuweka wazi kuwa ameamini wapinzani wao hao kuwafunga wakiwa uwanja wao wa nyumbani, ufanye kazi kubwa sana.

Chevalier alisema mbali ya ubora wa kikosi cha Simba, wamekuwa na nguvu kubwa ya mashabiki ambao amekiri walikuwa na mchango mkubwa kwenye ushindi waliopata.

Jumapili, Simba ikiwa Uwanja wa Mkapa, Dar, iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya ASEC Mimosas ukiwa ni mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika Kundi D.

Chevalier alisema: “Kusema ukweli Simba walikuwa wanastahili kushinda dhidi yetu kutokana na ubora mkubwa wa kikosi chao na nguvu yao wakiwa wanacheza nyumbani.

“Tulijitahidi kutumia mbinu na mipango yetu, lakini hatukufanikiwa, mashabiki wao walikuwa msaada mkubwa kwao wakiongezewa hamasa.

“Wachezaji wangu wengi vijana, kelele ziliwaathiri kwa sababu wamekaa miaka miwili bila uwepo wa mashabiki viwanjani kutokana na corona.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live