Kocha wa ASEC Mimosas, Julien Chevalier amewaangushia lawama wachezaji wake baada ya kushindwa kuifunga Timu ya Simba licha ya kutengeneza nafasi nyingi ambazo zilisalia kiduchu kuwa mabao.
Julien Chevalier amesema hayo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa hatua ya Makundi ya Kombe la Mabingwa Afrika ambapo Simba wakiwa nyumbani katika Dimba la Mkapa walitoa sare ya bao 1-1.
"Imetuchukua muda sana kurejea kwenye haya mashindano kwa sasa bado tunajipanga ukiangalia tumetoa wachezaji wengi sana ndani ya misimu miwili.
"Naweza kusema tulistahili ushindi kutokana na nafasi tulizotengeneza lakini sio mbaya kupata alama moja ugenini ni nzuri kwa kuanzia.
"Mechi yetu dhidi ya Wydad ndio mechi ambayo itaamua na sisi kujua zaidi wapi nafasi yetu ipo," amesema Julien Chevalier.