Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kocha APR alia na ratiba Mapinduzi Cup

Kocha APR Kocha APR alia na ratiba Mapinduzi Cup

Mon, 1 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa timu ya APR ya nchini Rwanda, Thierry Froger amesema kuna umuhimu mkubwa kwa wandaaji wa Kombe la Mapinduzi kutengeza mazingira bora zaidi ya uandaaji wa kombe hilo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari visiwani Zanzibar leo Desemba 31.

Amesema ni kinyume na utaratibu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) timu kila baada ya siku mbili kucheza mechi tena isiyokua ya kirafiki.

"Sisi tunacheza lakini tunavunjika moyo tunashindwa kujipanga na kuwa wazuri zaidi," amesema Froger

Akizungumzia kuhusu mchezo wa kesho dhidi ya wapinzani wao Singida Fountain Gate amesema anafahamu ni timu bora lakini wao ni bora zaidi.

Amesema katika mechi yao iliopita Singida FG ilishinda mabao 4-1 na anajua uwezo wao lakini wana mbinu zaidi ya wao.

Akizungumiza kuhusu mikakati ya kuchukua ubingwa wa kombe hilo kwa awamu hii ya msimu wa 18 amesema wanatamani na wataonyesha uwezo wao wote.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo, Sharaf Shiboub amesema hakuna kitu kigeni kwake kwenye soka la Tanzania kwakuwa anafahamu vyema kombe la Mapinduzi na karibu timu zote za Tanzania na anaamini timu yao itashinda.

Timu ya APR itaingia dimbani kwa mara ya kwanza leo Januari Mosi, 2024 ikicheza dhidi ya Singida saa 10:15 jioni.

Chanzo: Mwanaspoti