Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp yamkuta tena EPL

Jurgen Klopp Changes.jpeg Klopp yamkuta tena EPL

Mon, 25 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mamlaka inayoendesha Ligi Kuu England imefanya mabadiliko kadhaa kwenye ratiba ya ligi hiyo ambayo inaonekana kwenda kuwapa tabu Liverpool.

Vijana hao wa Jurgen Klopp watakuwa na kibarua cha kucheza mechi tatu za ugenini ndani ya siku sita huku mchezo mmoja wa Jumamosi ukitarajiwa kupigwa saa 6:30 mchana kwa saa za England, sawa na saa 9:30 alasiri kwa saa za Afrika Mashariki.

Safari ngumu kwa Liverpool itaanza Aprili 21 na ikisafiri hadi London kucheza na Fulham saa 1:30 usiku, kabla ya kurudi Liverpool kuvaana na watani zao wa jadi, Everton Aprili 24, kwenye Mercyside Dabi, kwenye Uwanja wa Goodison Park saa 5:00 usiku.

Mwisho itakutana na West Ham na itarudi London Aprili 27, mchezo utakaopigwa kuanza saa 9:30 alasiri.

Hivi karibuni Jurgen Klopp alilalamika kuhusu kuchezeshwa mechi za mapema hususani za Jumamosi na kwa ratiba hii ni wazi itamkera ukizingatia bado timu yake ipo kwenye michuano ya Europa League wanayocheza kila Alhamisi, hivyo huwa wanapata muda mchache sana wa kujiandaa.

Timu nyingine zinazoonekana kuwa na ratiba ngumu kidogo ni Arsenal ambayo itakuwa na mechi tatu ndani ya siku nane.

Itaanza dhidi ya Wolves Aprili 20, kabla ya kukutana na Chelsea Aprili 23 na kisha itaumana na Tottenham katika London Dabi Aprili 28.

Inaelezwa mabadiliko haya yamefanywa kutokana na ratiba za urushaji wa matangazo.

Chanzo: Mwanaspoti