Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp hataki kuvunja likizo

Lfc Foundation Klopp Ambassador Cover 090724 Jurgen Klopp

Sat, 3 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Jurgen Klopp amefichua kwamba hana mpango wa kurejea kwenye kazi ya ukocha kwa siku za hivi karibuni baada ya kuachana na Liverpool mwishoni mwa msimu uliopita.

Klopp, 57, alipata sifa kubwa kwa miaka yake tisa aliyokuwa kwenye kikosi hicho cha Anfield na kutwaa mataji kibao ikiwamo Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mjerumani huyo tangu ang'atuke Anfield amekuwa akihusishwa na dili kubwa kibao, ikiwamo ya kwenda kuinoa timu ya taifa ya England baada ya Gareth Southgate kung'oka zilipomalizika fainali za Euro 2024.

Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund aliweka wazi hana mpango wa kurudi kwenye kazi hiyo yenye presha nyingi hivi karibuni.

Klopp alisema atapenda kufanya mambo ya soka katika wigo tofauti, alisema: "Nikiwa kama kocha, sikung'atuka kwa kushinikizwa, ni kitu nilichokifanyia uamuzi. Nilipata nafasi ya kuzinoa klabu bora duniani.

"Pengine tunaweza kuzungumzia hilo tena miezi kadhaa ijayo. Bado nataka kufanya kazi kwenye soka kuwasaidia watu kutokana na uzoefu wangu. Ngoja tuone. Kwa kipindi hiki sitaki kitu kuhusu kazi ya ukocha. Si klabu wala timu ya taifa."

Kwa sasa, Klopp anafurahia maisha yake kwenye makazi yake mapya huko Majorca, Hispania, anakomiliki jumla la Pauni 3.4 milioni, sambamba na mkewe mrembo Ulla Sandrock. Kubwa ambalo Klopp amesisitiza kwamba hajastaafu ishu ya soka.

Chanzo: Mwanaspoti