Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp awasubiri mane na Salah awaweke kikao

SALAH MANE ohammed Salah, Kocha Jurgeni Klopp na Sadio Mane wa Liverpool

Tue, 8 Feb 2022 Chanzo: eatv.tv

Nahodha wa timu ya Egypt, Mohammed Salah amejiunga na klabu yake ya Liverpool leo Februari 8, 2022 na kuna uwezekano mkubwa wa kuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kwwenye mchezo wa EPL dhidi ya Leicester City Alhamis ya Februari 10, 2022.

Kwa Upande mwingiine,  Nahodha wa Senegal, Sadio Mane ambaye ametwaa ubingwa wa AFCON naye anatarajiwa kurejea klabuni hapo Jumatano au ya Alhamis wiki hii kukutana na mshambuliaji mwenzake Mohammed Salah ambaye alicheza walikuwa wapinzani kwenye fainali ya AFCON Februari 7, 2022 Nchini Cameroon.

Naye Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp aliweka wazi kuwa ataongea na wachezaji hao pindi watakaporejea baada ya kumalizika michuano ya AFCON ili kuwasahaulisha yaliyojiri katika kombe la mataifa ya Africa walipokua wapinznai hasa kwenye mchezo wa fainali ambapo Mohammed Salah alionekana kuumia sanaa baada ya kukosa ubingwa huo.

Kipindi ambacho Mane na Salah walikua kwenye majukumu ya timu zao za taifa katika michuano ya AFCON, Liverpool ilicheza michezo sita kwenye michuano yote na wameshinda michezo yote ikiwemo michezo miwili ya ligi kuu ya England na pamoja na michezo miwili ya nusu fainali ya kombe la carabao dhidi ya Arsenal.

Chanzo: eatv.tv