Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp aunga mkono kufutwa kwa VAR Ligi Kuu England

Jurgen Klopp Liverpool Scaled.jpeg Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp ameunga mkono kuondolewa kwa matumizi ya V.A.R kwenye michezo ya Ligi kuu nchini England msimu ujao.

Klopp ameeleza kuwa inavyotumika V.A.R sio kama vile ilivyotakiwa kutumika.Watu wanaoiendesha hawaiendeshi kama inavyotakiwa huku akisisitiza kuwa V.A.R sio tatizo ila watu wanaoiongoza.

"Namna inavyotumika kiuhalisia sio sahihi, namna wanavyoitumia.Naweza kupiga kura ya kuikataa."

"Hawa watu hawawezi kuiongoza vizuri. V.A.R sio tatizo, hauwezi kuwabadilisha watu hivyo naweza kupiga kura ya kuikataa V.A.R." Jurgen Klopp, kocha mkuu wa klabu ya Liverpool.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live