Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp atishwa na ugumu wa ratiba wakati huu wa Christmas

Maxresdefault 1 Jurgen Klopp

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha mkuu wa klabu ya liverpool, Jurgen Klopp amenukuliwa akisema kuwa ratiba ya michezo ya Christmas haiko sawa lakini anaukubali utamaduni huo wa michezo kufuatana kipindi cha Christmas.

Liverpool watawakaribisha klabu ya Leeds United tarehe 26 Disemba kwenye mchezo wa ligi kuu ya Uingereza siku ya Boxing Day, kabla ya kusafiri siku mbili baadae kwenda kwenye dimba la King Power Stadium kucheza na klabu ya Leicester City tarehe 28 Disemba.

“Disemba mara zote umekuwa ni mgumu, kila kitu kinakuwa sawa mpaka Christmas, tarehe 26/28, si sawa kucheza, tunakubali hilo, tunacheza, ila ni utamaduni lakini kwa kweli ni mgumu sana, January sio mwezi mzuri maana muda mwingi unakuwa kwenye makombe ni sawa na Disemba, kwaiyo tuna miezi miwili migumu mbele yetu.” Klopp

Siku ya Jumapili klabu ya Liverpool wanasafiri hadi kwenye jiji la Wolverhampton kuwavaa Wolverhampton Wanderers kwenye dimba la Molineux Stadium kuendeleza wimbi la ushindi kama watapata nafasi kuondoka na pointi tatu baada ya kutoa kichapo kwa Everton.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live