Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp ateta na Salah suala la Mkataba mpya

Salah Na Klopp Mohammed Salah akiwa na Klopp

Tue, 7 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kwa namna ambavyo amekuwa akiishi na fowadi wa kimataifa wa Misri na klabu hiyo Mohamed Salah anamatumaini ataongeza mkataba kabla ya huu wa sasa haujamalizika.

Mchezaji huyo ambaye kwa sasa yuko kwenye kiwango bora kabisa kiasi cha kuongoza kwa kupachika mabao ndani ya EPL akiwa na goli 13 katika takribani mechi nane pekee.

Salah, 29, ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Roma mwaka 2017 mkataba wake unamalizika mwishoni mwa mwezi Juni mwakani.

“Tunazungumza pamoja, kuongeza mkataba kwa mchezaji wa kariba ya Salah siyo sawa na kitendo cha kuweka maji kwenye gesi na kuweka rangi kisha unywe chai, ni mchakato” alisema kocha huyo.

Ameongeza pia kuwa: “Mo yuko sawa, mimi niko poa, tunalolihitaji ni kuhakikisha tunalolihitaji linafikiwa”.

Liverpool watacheza na AC Milan kesho Jumanne katika mchezo wa kukamilisha ratiba baada ya kufuzu kwenye mechi nne zilizopita ambapo mchezo huo umepangwa kuchezwa na kikosi cha vijana.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live