Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp apigwa faini milioni 81

Jurgen Klopp Handa Up Klopp apigwa faini milioni 81

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amepigwa adhabu ya kulipa faini £30,000 (Tsh milioni 81) kwa kosa la kugombana na Mwamuzi kwenye Mechi dhidi ya Man City, Oktoba 16, 2022 baada ya Mohamed Salah kunyimwa faulo.

Shirikisho la Soka (FA) limempa adhabu hiyo Meneja wa Liverpool kwa kosa la kugombana na mwamuzi msaidizi kwenye mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester City ambapo Liverpool walishinda kwa bao 1-0.

Klopp, alioneshwa kadi nyekundu kwa kujibizana na Mwamuzi baada ya Mohamed Salah kunyimwa mpira wa adhabu kwenye mechi iliyochezwa Oktoba 16, 2022.

Meneja huyo aliomba radhi kwa tabia aliyoonesha na kusema alipaswa kukabiliana na hali hiyo. Liverpool, inayoshika nafasi ya 8 Ligi Kuu itacheza na Leeds United Jumamosi Oktoba 29.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live