Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp anaondoka!

Clop Pic Data Klopp anaondoka!

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

SIKU zinakwenda kasi sana. Ghafla tu mambo yamebadili na Jurgen Klopp amekuwa miongoni mwa makocha wanaoweza kufunguliwa mlango wa kutokea kwenye Ligi Kuu England muda wowote.

Wacheza kamari wameanza kubeti kwamba kocha huyo wa Liverpool anaweza kuwa ndiye anayefuata kwenye kufutwa kazi baada ya miamba hiyo ya Anfield kukumbana na kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa Leicester City katika kipute kilichopigwa King Power.

Liverpool waliokuwa wakipewa nafasi za kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England wiki kadhaa zilizopita, sasa wamekuwa wepesi kuliko maelezo wapinzani wanajipigia tu, huku kichapo hicho cha uwanjani King Power kikiwatoa kabisa kwenye ramani za kukimbizia ubingwa wa msimu huu.

Hata kocha mwenyewe, Klopp amekiri kwamba sasa suala la ubingwa itakuwa ndoto za mchana kwao kama wataendelea kuamini atalinyakua taji hilo kwa msimu huu.

Klopp, aliyeiongoza Liverpool kubeba Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu England misimu miwili iliyopita, alikuwa na 10/1 kwenye uwezekano wa kufutwa kazi huko Anfield kabla ya mechi hiyo ya kipigo kutoka kwa vijana wa Brendan Rodgers.

Lakini, baada ya James Maddison, Jamie Vardy na Harvey Barnes kufunga na kulifuta lile bao la utangulizi la Liverpool lilifungwa na Mohamed Salah, mambo yalibadilika na Klopp amepewa 4/7 ikiwa ni kwamba ana nafasi kubwa ya kufutwa kazi. Hiyo ni kwamba kuna nafasi nne kati ya saba za uwezekano wa Mjerumani huyo kufungashiwa virago vyake huko Anfield kulingana na mwenendo wa timu yake.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz