Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp amwaga Sifa kwa Kelleher

Kelleher.jpeg Caoimhin Kelleher

Mon, 28 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemmwagia sifa goli kipa Caoimhin Caoimhin Kelleher kwa kucheza dakika 120 bila kuruhusu bao lakini pia kufunga penati iliyoipa ushindi Liverpool wa penati 11 kwa 10 dhidi ya Chelsea kwenye mchezo wa fainali ya Carabao CUP.

Caoimhin Kelleher mwenye umri wa miaka 23 alipewa nafasi ya kuanza kwenye mchezo huo wa fainali mbele ya golikipa namba moja Alisson Becker , ingawa kwenye michuano Carabao Kelleher ndio alikuwa chagua la kwanza kwenye michezo mingi.

Baada ya mchezo huo kocha Jurgen Klopp akamwagia sifa golikipa huyu kinda raia wa Ireland, hususani kwa kumuamini na kumpa nafasi ya kuanza mbele ya Becker kwenye mchezo mkubwa wa Fainali dhidi ya timu kubwa kama Chelsea,

"Hata katika soka la kulipwa kunapaswa kuwa na nafasi ya hisia. Caoimhin Kelleher ni kijana mdogo, anacheza katika mashindano yote, nifanye nini? Mimi nina vitu viwili, Meneja kitaaluma na ni binadamu na ubinadamu umeshinda. Alistahili.” Amesema klopp.

Kwenye mchezo huo wa fainali timu hizo zilifika hatua ya kupigiana penati baada ya kucheza dakika 120 bila kufungana na kwenye changamoto ya mikwaju ya penati Liverpool walipata penati zao zote 11 wakati golikipa wa Chelsea Kepa Arrizabalaga ambaye aliingia mahususi kwa ajaili ya penati alishindwa kudaka penati hata moja na akakosa penati kwa upande wa Chelesea na kuipa Liverpool kombe la kwanza la msimu na ubingwa wao wa 9 wa michuano hii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live