Jurgen Klopp amemtaja Sadio Mane kama “mchezaji wa kiwango cha dunia” na akasema kuwa na wakati wa kupumzika baada ya msimu uliopita kumekuwa maana katika kiwango chake cha hivi karibuni.
Mshambuliji huyo wa Liverpool anashika nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu ya England pamoja na Jamie Vardy wa Leicester City wenye mabao saba, ni mchezaji mwenzake Mohammed Salah pekee aliye na zaidi (11).
Baada ya misimu mizuri Anfield, Mane hakuwa katika ubora wake 2020-21. Ingawa bado alimaliza akiwa na mabao 16 katika michuano yote, idadi hiyo ilikuwa ya chini zaidi tangu alipocheza kwa mara ya kwanza akiwa na Liverpool (13 msimu 2016-17).
Hata hivyo, Mane sasa anaonekana kurejea katika ubora wake na, kabla ya kukabiliana na klabu ya fowadi huyo wa zamani wa Senegal, Southampton, Klopp alitabiri kampeni nyingine bora kwa mchezaji huyo wa miaka 29 mradi tu asipate majeraha.
“Nadhani tunaweza kumuits Sadio kama mchezaji wa kiwango cha dunia.Unaona namba Mo ana mabao 108 [kwa jumla katika Premier League] na Sadio ana mabao 102 mengi akiwa na Liverpool, lakini ni wazi baadhi akiwa na Southampton.
“Sadio ni mtu anayejiamini sana na alijua, sote tulihisi siku ya kwanza ya maandalizi ya msimu, baada ya mapumziko sahihi, alikuwa hapo kwa asilimia 100. Ilikuwa wazi.