Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp amuombea njaa Salah AFCON

Kloppsalahendo 1 Klopp amuombea njaa Salah AFCON

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Roho Mbaya! Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hamuombei mema mchezaji wake Mohamed Salah kuelekea mashindano ya Mataifa ya Afrika ‘AFCON’ yanayotarajiwa kuanza Ivory Coast kuanzia Januari 13.

Salah atakuwa nje ya kikosi cha Liverpool kwa ajili ya kulitumikia taifa lake la Misri kwenye AFCON, vilevile Wataru Endo ambaye ni kapteni wa Timu ya Taifa ya Japan atakuwa kwenye majukumu ya timu hiyo kwenye mashindano ya Asian Cup yatakayofanyika Qatar kuanzia Januari 12.

Ikiwa mataifa ya wachezaji hawa yatafanya vizuri kwenye mashindano haya, Liverpool italazimika kusubiri hadi wiki ya pili ya Februari mwaka huu ili kupata huduma zao.

Hii ndio sababu Klopp kufichua kwamba hawatakii mema na anaombea watolewe mapema ili zaidi ni kuona wanarudi wakiwa wazima tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live