Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp ammwagia sifa Trent Arnold idara ya Ulinzi

Trent Body Klopp ammwagia sifa Trent Arnold idara ya Ulinzi

Sat, 31 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amemsifu Trent Alexander-Arnold kutokana na kiwango bora alichoonesha eneo la ulinzi kwa Harvey Barnes katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Leicester City hapo jana.

The Reds walipata ushindi wao wa nne mfululizo wa ligi na kubakiza pointi mbili mbele dhidi ya Tottenham walio katika nafasi ya nne huku wakijaribu kuokoa kampeni yao baada ya kuanza msimu kwa kusuasua.

Mabao mawili ya kujifunga kutoka kwa Wout Faes mwishoni mwa kipindi cha kwanza yaliipatia Liverpool pointi tatu baada ya Kiernan Dewsbury-Hall kupenya katikati ya safu ya ulinzi ya Reds na kutangulia kufunga dakika ya nne.

Alexander-Arnold, ambaye amekuwa na msimu mbovu, amepokea sifa kutoka kwa Klopp huku Wekundu hao wakiwazuia Foxes, na kuzima tishio la Barnes kwenye upande wa kushoto wa Leicester.

Klopp alisema; “Nzuri sana, na sio mara ya kwanza, ilikuwa nzuri sana, inasaidia sana na muhimu sana katika nyakati hizi. Inasaidia sana, na nadhani kila mtu anajua jinsi Harvey Barnes alivyo mzuri katika hizi na Trent alifanya vizuri sana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live