Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp amchimba mkwara mzito Darwin Nunez

Skysports Nunez Klopp 5865060 Klopp amchimba mkwara mzito Darwin Nunez

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kwamba Darwin Nunez anatakiwa akazane kama anataka kuanza kikosi cha kwanza msimu ujao.

Licha ya straika huyo kuonyesha kiwango bora kwenye mechi za pre season na kufunga bao dhidi ya Leicester City na baadaye kufunga mabao mawili walipocheza dhidi ya Greuther Furth bado anatakiwa aongeze juhudi

“Nunez anatakiwa pia kukaba kwani ni njia ya mafanikio pia, alinipa matumaini msimu uliopita. Lakini majeraha, kadi nyekundu mwanzoni hazikumsaidia kabisa.

Najuwa ubora wa wachezaji kwani Nunez anapokuwa mazoezini anakuwa na kiwango bora sana, kuwa fiti inasaidia sana ngoja tuone baada ya mechi mbili za mwanzo za ligi nini kitatokea.” alisema Klopp.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live