Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp alia na Waarabu

Jurgen Klopp Changes.jpeg Klopp alia na Waarabu

Thu, 3 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amelalamikia namna ambavyo klabu za Saudi Arabia zinamwaga pesa kwa ajili ya kusajili wachezaji.

Klopp ameenda mbali na kusema, anguko la klabu za Ulaya linaanza kutengenezwa na Ligi ya Saudi Arabia. Ameomba UEFA na FIFA kutafuta suluhu ya hili jambo.

Kitu kingine anacholalamikia Klopp ni dirisha la usajili Saudi Arabia kufungwa mwezi Septemba 20 wakati nchi nyingi za Ulaya madirisha ya usajili yanafungwa Septemba 1.

Anachokiona Klopp ni kwamba, wakati dirisha la usajili Ulaya limefungwa, Saudi Arabia watakuwa bado wanaweza kusajili! Hofu yake ni klabu za Saudi Arabia bado zitaweza kusajili wachezaji kutoka Ulaya.

Kwa hiyo wakati makocha wa klabu za Ulaya wakiwa wanaamini kikosi chake ni hiki kwa ajili ya msimu husika, inawezekana sasa klabu za Saudi Arabia zikachomoa wachezaji Ulaya kwa sababu dirisha lao la usajili litakuwa wazi.

Sasa @edgarkibwana amepingana na madai ya Klopp, Edgar amesema goli liachwe wazi mwenye kisu kikali ndio ale nyama.

“Kwa upande wangu naona mwenye kisu kikali aachwe ale nyama, kaulimbiu ya FIFA ni mpira usambae, haya maneno ya kina Klopp ni namna tu ya kujitetea, wapunguze uoga washindane.”

“Kwanza Ulaya wanajinasibu kwamba UEFA Champions League ndio ina mzigo mrefu wa maokoto, ndio ligi bora kwa maana ya ushindani sasa waiache dunia izungumze kwa namna yake na wakubali kushindana.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live