Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp ajutia hili Liverpool

Jurgen Klopp Vvs Tadic Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp ameweka wazi kuwa anajuta kutokumsajiri nyota wa klabu ya Ajax Dusan Tadic kwenye klabu ya yake ya Liverpool baada ya kuwa na nafasi ya kufanya hivyo.

Tadic anatarajia kukutana na Jurgen Klopp leo kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa, ambapo Ajax watawakaribisha klabu ya liverpool kwenye jiji la Amsterdam kwenye usiku wa Ulaya.

Tadic alijiunga na klabu ya Ajax kwenye majira ya kiangazi mwaka 2018 kutokea klabu ya ya Southampton, baada ya kuwa na misimu minne bora kwenye klabu hiyo, kabla ya kwenye nchini uhalonzi ambapo aliundeleza moto wake.

Mpaka sasa Dusan Tadic amefanikiwa kufunga magoli 94, huku akisaidia kupatikana kwa magoli 98 kwenye michezo 209 aliyoichezea klabu hiyo, pia amekuwa na mchango mkubwa kwenye mataji matatu walichoshinda na kufanikiwa kuifikisha Ajax kwenye nusu fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2019.

Kuelekea mchezo wa jana, jurgen Klopp ameweka wazi hasira yake kwa kushindwa kumsajiri mchezi huyo mwenye miaka 33 sasa, kwa kuikiambia RTL: “Nampenda Tadic kama mchezaji.

“Nilikuwa na hasira dhidi yangu pale Tadic aliposajiliwa na klabu ya Ajax, kwa sababu nilikuwa navutiwa nae”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live