Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp aikoromea Bodi ya Ligi

Jurgen Klopp Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ameikashifu Bodi ya Ligi Kuu England na televisheni kwa kupanga mechi yao muhimu dhidi ya Manchester City baada ya mapumziko ya kimataifa, kwenye Uwanja wa Anfield.

Mechi hiyo itakayochezwa itarushwa na Kituo cha Televisheni cha Sky Sports mchana Novemba 25 zaidi ya saa 72, ambapo wachezaji wote watakuwa wanamaliza mechi za kufuzu Kombe la Dunia kutoka Mataifa ya Amerika ya Kusini ikiwa ni pamoja na mechi ya Brazil na Argentina kwani umbali wake utakuwa zaidi zaidi ya kilometa 6,000.

Mastaa kama Ederson, Alisson, Julian Alvarez, Alexis Mac Allister na Darwin Nunez watakuwa wataathirika zaidi.

Akiongea kwa hasira Klopp alisema: “Unawezaje kupanga mechi kama hiyo saa 12:30 mchana? Kusema kweli, watu wanaofanya maamuzi watakuwa hawajui soka. Haiwezekani kitu kama hiki. Watu duniani kote wamejipanga zaidi kuona mchezo wa soka kama huo halafu mambo kama haya yanatokea. Wachezaji wa Amerika ya Kusini watakuwa kwenye ndege wakirudi kwa ajili ya kuwahi mechi, ina maana ndege itawachukua kutoka nchi tofauti?”

Klopp anaamini maamuzi hayo yatawaathiri baadhi ya wachezaji ambao watarudi wakiwa wamechoka sana na hawataonyesha viwango bora kwenye mechi hiyo muhimu kwenye ligi.

“Lazima upambane katika ligi ngumu zaidi kama hiyo, wachezaji wanatakiwa kuwa tayari kujiandaa na mechi kuanzia Alhamisi na Jumapili na Alhamisi. Hivyo kabla ya Jumamosi saa 12:30 mchana wachezaji wa wanatakiwa kuwa fiti asilimia 100.”

Mara kwa mara Klopp amekuwa akilalamikia ratiba za mechi ya mchana, ikiwa ni pamoja na mjadala mkali na mwandishi wa habari Des Kelly mwaka 2020, baada ya kukubali bao la dakika za mwisho katika sare ya 1-1 na Brighton kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu England iliyochezwa mchana. Pia, Klopp alifadhaishwa mwaka 2022 wakati Liverpool ilipopangwa kuvaana na Newcastle mapema Jumamosi katikati ya mechi yao ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Villarreal.

Angalau kikosi cha Klopp kitaingia kwenye mechi dhidi ya City kwa kujiamini kwani kimeshinda mechi 18 mfululizo ikiondoa sare dhidi ya Luton Town kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Brentford 3-0 wikiendi iliyopita.

Chanzo: Mwanaspoti