Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp achekelea Mateso ya Chelsea

Jurgen Klopp Winner Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp

Thu, 4 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema anafurahia kuwaona Chelsea wakiteseka kwa vichapo licha ya kufanya usajili mkubwa na mastaa wa maana.

Klopp amesema:

“Najisikia furaha kuhusu Chelsea kusema ukweli, kwa sababu hawafanyi vizuri. Wao ni timu kubwa, lakini kwa upande mwingine ni vizuri kutambua si tu unaleta wachezaji wa kiwango cha juu na kuwaweka pamoja, unapaswa ufikirie wataendana.

“Huwezi kuwa na vyumba viwili vya kubadilishia, huwezi kufanya mazoezi kwenye viwanja viwili, lazima utengeneze uhusiano, utengeneze ari na hilo si jambo rahisi ndio maana nafurahi juu ya hilo. Lazima ulete wachezaji sahihi kwa ajili ya kujenga timu. Hilo ndo ambalo sisi hatuwezi kufanya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: