Sun, 22 Jan 2023
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp baada ya kutoka sare tasa ya bila kufungana na Chelsea amedai kuwa ameyapokea kwa moyo mmoja matokeo hayo.
Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari, Klopp amesema kuwa Arsene Wenger aliwahi kufungwa 6-0 kwenye mchezo wake wa 1,000 hivyo kwake sare ya 0-0 anafurahi.
“Nimesikia Arsene Wenger alipoteza mchezo wake wa 1,000 kwa 6-0 , ninafuraha hayakunitokea,” amesema Klopp.
Mechi ambayo Jurgen Klopp amekumbushia ni ya mwaka 2014, wakati Chelsea ikiongozwa na Jose Mourinho na kuifunga Arsenal magoli 6-0.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live