Kocha mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp ameitaka timu yake kubaki makini na jukumu lililo mkononi wakati wanajipanga kupindua meza Ligi ya Mabingwa na kusahau jinsi walivyoichakaza Manchester United.
Ushindi wa kusisimua wa mabao 7-0 kwenye Uwanja wa Anfield Jumapili iliyopita uliongeza matumaini mengine kwa Liverpool walio katika nafasi ya tano na ushindi dhidi ya Bournemouth katika mechi ya mapema Jumamosi utawafanya waipeperushe Tottenham kwa muda katika nafasi ya nne.
Liverpool wanaelekea pwani ya kusini huku matokeo ya wikendi iliyopita yakiwa yangali mbele ya akili za wengi lakini Klopp aliweka wazi ushindi wa zamani, hata ukiwa na msisitizo kiasi gani, sio muhimu tena.
Klopp anafahamu Bournemouth itatoa changamoto kubwa kwa timu yake, baada ya kuongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya vinara wa ligi Arsenal mara ya mwisho kabla ya kurejea tena kipindi cha pili kutoka kwa The Gunners.
Huku kushuka daraja bado ni tishio kwa Cherries, Klopp anatarajia wenyeji “kupigana kama wazimu huku akikazia kuwa jambo kuu ni kwenda Bournemouth na kucheza mchezo bila kuhesabu pointi kabla ya kuwa nazo.
“Jinsi Bournemouth wanavyocheza, wanaweza kukosa raha kwa kila timu kila mtu aliona dhidi ya Arsenal katika mchezo uliopita, ni kiasi gani walilazimika kupigana na kunyoosha bahati.”
Tunaweza kupigania nafasi za Ligi ya Mabingwa tutaona jinsi matokeo yatakavyokuwa wiki chache zijazo lakini pambano la kusalia kwenye ligi ni la kusisimua. Bournemouth watapambana kama wazimu. Tunataka kuingia katika nafasi nne za juu, lakini ni kuhusu kuangazia Bournemouth kikamilifu. Alisema Klopp.