Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp: Tumepigwa, hakuna shida

Jurgen Klopp Handa Up Klopp: Tumepigwa, hakuna shida

Fri, 12 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Liverpool imepoteza kwa mabao 3-0 ikiwa nyumbani dhidi ya Atalanta katika mchezo wa Europa League hatua ya robo fainali uliochezwa Anfield, jana usiku, huku kocha wao Jurgen Klopp akisema hakuna presha kwenye timu hiyo.

Mshambuliaji wa zamani wa West Ham United, Gianluca Scamacca, alifungua karamu ya mabao dakika ya 38, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 60.

Licha ya Klopp kuwaingiza kipindi cha pili Mohamed Salah, Dominik Szoboszlai, Robertson na Luis Diaz ili kuweka mambo sawa, lakini walijikuta wakipigwa msumari wa tatu dakika ya 83, mfungaji akiwa Mario Pasalic.

Kutokana na matokeo hayo, sasa Liverpool inatakiwa kwenda ugenini Aprili 18, mwaka huu kupindua meza ili kufuzu nusu fainali ikitakiwa kupata ushindi wa mabao 4-0.

Kichapo hicho ni cha kwanza kwa Liverpool kukipata nyumbani katika michuano ya Ulaya tangu mara ya mwisho wafungwe 5-2 na Real Madrid, Februari 21, mwaka 2023.

Pia hicho ni kipigo cha tatu kikubwa Liverpool kukipata nyumbani kwenye michuano ya Ulaya, baada ya Oktoba 12, mwaka 2014 kufungwa 3-0 dhidi ya Real Madrid.

"Hakuna presha na sioni kama nina jambo ninaloweza kulijutia kwa sasa, tulicheza vizuri tumepoteza hakuna jambo lingine, nafikiri tunatakiwa kuwaza mchezo ujao," alisema Klopp.

Mechi nyingine ilishuhudia West Ham ikilala kwa mabao 2-0 dhidi ya Bayern Leverkusen, AC Milan ikachapwa na Roma 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live