Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp: Sina wasiwasi na Liverpool

Jurgen Klopp Liverpool Scaled.jpeg Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema hana presha juu ya hatma ya Liverpool msimu ujao licha ya kwamba atakuwa nje ya timu hiyo.

Klopp alitangaza ataondoka Liverpool ifikapo mwisho wa msimu huu ikiwa ni baada ya kuhudumu kwenye timu hiyo tangu mwaka 2015.

Msimu huu pia ameshabeba taji moja ya Carabao ilipoichapa Chelsea bao 1-0 kwenye Uwanja wa Wembley na Jumapili atakuwa akiiongoza Majogoo wa Liverpool kwenye mchezo wa Kombe la FA ugenini kwenye Uwanja wa Old Trafford dhidi ya Manchester United.

Klopp anataka kuondoka klabuni hapo akiwa na mataji na anapambana kuhakikisha anabeba yaliyo mbele yake kabla msimu haujamalizika huku pia akiwa kwenye michuano ya Europa League na leo usiku itashuka uwanjani dhidi ya Sparta Prague kwenye mchezo wa marudiano baada ya awali kushinda mabao 5-0 ugenini Jamuhuri ya Czech.

Ameiongoza Liver kutwaa taji moja la Ligi Kuu msimu wa 2019/20 na msimu huu iko kwenye mbio za ubingwa ikiwania taji la pili kwa kocha huyo raia wa Ujerumani.

Kocha huyu ambaye amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Liverpool, aliwaambia mabosi wa timu hiyo juu ya uamuzi wao huo Novemba mwaka jana sababu kubwa ikiwa ni kutaka kupumzika baada ya kuhudumu kwa muda mrefu.

Wakati huo huo, inaelezwa Pepijn Lijnders, Peter Krawietz na Vitor Matos ambao ni sehemu ya benchi lake la ufundi pia wataondoka.

Alipoulizwa wakati wa mahojiano kabla ya mchezo wao huo wa leo Klopp amesema;

"Sina wasiwasi wowote kwa sababu timu ipo vizuri kiushindani na ipo kwenye nafasi nzuri kwa sasa na hapo baadaye inategemea na aina ya wachezaji watakaokuwepo, uongozi na timu kwa jumla itakavyokuwa."

Klopp pia amesema ili Liverpool ifanye vizuri lazima uongozi uwe imara jambo ambalo linampa matumaini sana kwa sababu anaufahamu vizuri uongozi wa timu hiyo.

Katika kujiandaa na maisha bila ya Klopp, Liverpool imemrudisha Mkurugenzi wao wa zamani wa michezo, Michael Edwards ambaye amarejea katika nafasi hiyo.

Vigogo hao wamemrudisha Edward kwa sababu yeye ndio alikuwa nyuma ya mipango ya kuisuka Liverpool wakati Jurgen Klopp anaingia kwenye timu.

Klopp anaamini urejeo wa Edward pia unampa matumaini Liverpool itaendelea vizuri sana baada ya yeye kuondoka.

Chanzo: Mwanaspoti