Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp: Salah atarudi AFCON, mleteni apata matibabu

Skysports Klopp Salah 6430710 Klopp: Salah atarudi AFCON, mleteni apata matibabu

Fri, 26 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema mshambuliaji Mohamed Salah atarejea kwenye fainali za Mataifa ya Afrika kama atapona kwa wakati na Misri itafika fainali ya michuano hiyo.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 31 alirejea England kwa ajili ya matibabu baada ya kupata majeraha kwenye mchezo dhidi ya Ghana uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 wiki iliyopita.

Kocha msaidizi wa Liverpool, Pepijn Lijnders alisema Salah anatarajia kurejea uwanjari wiki tatu au nne zijazo kama hatajitonesha kwenye majeraha yake wakati akijiuguza.

“Misri na Liverpool wote wana malengo yanayofanana, tunamtaka Salah akiwa fiti kadiri inavyowezekana,” alisema Klopp baada ya timu yake kufika fainali ya Kombe la Ligi juzi Jumatano (Januari 24) kwa kuifunga Fulham.

“Kama atabaki Afrika na watashindwa kumpa matibabu sahihi, itachelewesha kila kitu hasa kwa Misri kama watafika mpaka hatua ya mwisho ya mashindano.

“Tumemleta hapa sio kwa sababu tunataka kumuondoa kwenye timu ya taifa ya Misri lakini kumpa matibabu bora.

“Wote tunakubali, kama Salah atakuwa fiti na Misri, iko wazi asilimia 100 atarejea kwenye timu ya taifa. Mo anataka hivyo, na sisi tunataka hivyo.”

Misri wanaoshikilia rekodi ya kushinda ubingwa wa Afrika mara saba walimaliza nafasi ya pili kwenye Kundi B baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 kwenye mechi tatu mfululizo.

Watakutana na timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kwenye hatua ya 16 bora Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live