Kocha wa klabu ya Liverpool raia wa kimataifa wa Ujerumani Jurgen Klopp amesema moyo wake upo ndani ya klabu hiyo na sio shemu nyingine yeyote kama ambavyo taarifa zingine zinasambaa.
Kocha Klopp amezungumza hayo baada ya kuulizwa kuhusiana na kutakiwa na shirikisho la soka nchini Ujerumani kwajili ya kuinoa timu ya taifa ya nchi hiyo ambapo kocha Hans Flick alitimuliwa siku kadhaa nyuma.
Kocha huyo amesisitiza kua licha ya kujitoa na kua mwaminifu kwajili ya Liverpool, Lakini anakumbuka miaka nane aliyokaa klabuni hapo kwakua sio kitu ambacho unaweza ukakiondoa tu mara moja.
Kocha huyo ameeleza zaidi ana mkataba ndani ya klabu ya Liverpool ambao amesaini siku kadhaa nyuma, Huku akisema wakati anasaini mkataba huo hakua amelewa au kufungwa alisaini kwa akiwa anajitambua hivo anachokiongea anaaminisha.
Jurgen Klopp hajioni akiondoka Liverpool siku za karibuni na majibu yake kuhusiana na kufundisha timu ya taifa ya Ujerumani yameonesha wazi kabisa kua kocha huyo ana mpango wa kuendelea kusalia ndani ya viunga vya Anfield kwa muda mrefu zaidi.