Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp: Mechi ijayo ni fainali

Liver Pic Data Klopp: Mechi ijayo ni fainali

Thu, 20 May 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LONDON, LIVERPOOL. KOCHA wa Liverpool, Jurgen Klopp ameufananisha mchezo waliocheza dhidi ya  Burnley kwa kusema ulikuwa kama nusu fainali kwao ya Ligi Kuu England huku kibarua kilichopo mbele yao dhidi ya Crystal Palace ndio fainali yenyewe.

Ushindi ambao waliupata Liverpool wikiendi iliyopita dhidi ya West Bromwich uliweka hai matumaini yao ya kumaliza msimu wakiwa kwenye nafasi nne bora ili msimu ujao wacheze Ligi ya Mabingwa kabla ya  kucheza dhidi ya Burnley.

Usiku wa jana, Jumatano, Liverpool wakiwa ugenini  kwenye uwanja wa Turf Moor  waliendeleza kile ambacho walikifanya wikiendi iliyopita kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wao, Burnley.

Mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Klopp alisema, "Leo (jana) ulikuwa mchezo wa nusu fainali na ilitakiwa tushinde na jambo zuri kwetu ni kwamba tumeshinda. Hakuna kitu muhimu zaidi kwetu kama kusogea nafasi za juu,"

"Tunatakiwa kuwa sawa na tayari kwa mchezo ujao ambao utakuwa kama fainali yetu. Nasubiri kuona tukicheza mbele ya mashabiki (10,000)  wetu tukiwa nyumbani, Anfield  itakuwa siku ya kipekee," alisema kocha huyo.

Ushindi ambao wameupata Liverpool dhidi ya Burnley huku mabao yao kwenye mchezo huo yakifungwa na Roberto Firmino,Nathaniel Phillips and Alex Oxlade-Chamberlain yameifanya timu hiyo kusogea hadi nafasi ya nne huku ikiishusha Leicester City kwenye nafasi hiyo licha ya kuwa na pointi sawa 66.

Liverpool imebebwa na utofauti wa mabao, pazia la Ligi Kuu England linatarajiwa kufungwa, Jumapili kwa michezo yote kuchezwa kwa muda mmoja, wakati Liverpool ikicheza dhidi ya  Crystal Palace, Leicester City watakuwa na kibarua cha kupepetana na Tottenham, Chelsea ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi 67 watakuwa ugenini kucheza dhidi ya Aston Villa.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz