Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amefunguka na kuweka hadharani hatima ya maisha yake huko Anfield baada ya chama lake kuchapwa Tatu Bila na Wolves katika mchezo wa Ligi Kuu England wikiendi iliyopita, akisisitiza ataweka mambo sawa.
Liverpool ilipigwa kirahisi sana huko Molineux Jumamosi iliyopita. Bao la kujifunga la Joel Matip liliwafanya Wolves kuongoza kabla ya staa wao mpya waliyemnasa Januari, Craig Dawson kupiga chuma cha pili na Ruben Neves akahakikisha ushindi huo kwa kufunga bao la tatu katika ushindi wa mabao 3-0 na hivyo Wolves kujiweka kwenye mazingira mazuri katika vita yao ya kukwepa kushuka daraja.
Liverpool hali ni mbaya, wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi 20 ambapo wamekusanya pointi 29. Mbaya zaidi haijaonja ushindi kwa mwaka huu wa 2023, wakipoteza mechi tatu na kutoka sare moja. Mara ya mwisho kushinda ilikuwa Desemba 28 dhidi ya Leicester.
Lakini, pamoja na mwendo huo wa hovyo, Klopp anaamini atarudisha timu hiyo kwenye makali yake, alipojibu swali la kama ataweza kunusuru hali ya mambo inayoendelea kwa sasa Liverpool, alise: “Yeah, yeah, yeah. Bila shaka.”
Alipoulizwa atawezaje kuirudisha Liverpool kwenye makali msimu huu, Klopp alisema:
“Hiyo sio kwenye mikutano ya waandishi. Haina maana. Unajua kazi yangu, najua kazi yangu na kazi yangu sio kuelezea hapa nitaweza kuijenga timu yangu. Nitahukumiwa kuanzia hapo, hilo sawa. Acha niishie hapo.” Mechi zijazo Liverpool
Februari 13 vs Evarton
Februari 18 vs Newcastle
Februari 21 vs Real Madrid
Februari 25 vs Crystal Palance
Mechi 5 vs Man United (nyumbani)