Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klopp, Guardiola,Ten Hag wakutana kwa Kimmich, nani kulamba dume?

Gfdxtfdxfc Klopp, Guardiola,Ten Hag wakutana kwa Kimmich, nani kulamba dume?

Tue, 26 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mancherster United imeungana na Manchester City na Liverpool kwenye mchakato wa kuiwania huduma ya kiungo wa Bayern Munich Joshua Kimmich, 28, kuelekea dirisha lijalo.

Kimmich ambaye ni mmoja kati ya wachezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Munich, anadaiwa kuwa hana mpango wa kuondoka Januari na badala yake atasubiri hadi mwisho wa msimu huu.

Timu nyingi zimevutiwa na staa huyu ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwaka 2025, kutokana na kiwango bora alichoonyesha tangu kuanza kwa msimu huu ambapo kwenye mechi 20 za michuano yote, amefunga bao moja na asisti sita.

Awali Barcelona na Manchester City ndio zilionekana kuwa na uhitaji zaidi wa staa huyu lakini hivi karibuni Man United inadaiwa kuanza mazungumzo na wakala wake kuangalia uwezekano wa kumsajili.

Kimmich, ambaye amejiunga na Bayern akitokea RB Leipzig mwaka 2015, kiujumla amecheza mechi 367, akifunga mabao 41 na kutoa asisti 100.

Chanzo: Mwanaspoti