Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp amesisitiza kwamba wameweka kando sakata la VAR na kusisitiza watu walimuelevwa vibaya aliposema mechi yao dhidi ya Tottenham irudiwe.
Kabla ya kucheza dhidi ya Union SG katika mechi ya Europa, Kocha huyo alisema anaamini kwamba mechi inastahili kurudiwa baada ya makosa kutokea mwishoni mwa juma lililopita.
Klopp alisema: “Mimi ni mtu wa soka nadhani mechi inastahili kurudiwa. Mabadiliko hayakutokea kabisa. Muhimu kwa sababu kila mtu ametazama kwa jicho la tofauti tusisahau kuhusu hilo.
Ikaelezwa pia kuwa fowadi wa Liverpool Diogo Jota alilimwa kadi nyekundu kimakosa baada ya kuangaliwa upya.
Hata hivyo, Klopp akabadili kauli yake akidai watu walimuelewa vibaya alipozungumza hivyo kwani wachezaji wake wamesahau majanga yaliyotokea katika kipigo cha 2-1 walichopata dhidi ya Spurs.
“Vizuri sana, unataka Jota afanyaje kuhusu hilo? Najua itakuwa ngumu sana, nilipozungumza kuhusu mechi ya Spurs, imenithibitishia jinsi dunia ilivyo,” Klopp aliongeza.
Baada ya kupokea kichapo cha kwanza katika Ligi Kuu England tangu msimu uliopita, Klopp alifanya mabadiliko ya wachezaji tisa ambao walicheza dhidi ya Union SG juzi Alhamisi (Oktoba 05).
Kikosi cha Liverpool kilikwa hatari na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 yaliyowekwa kimiani na Ryan Gravenberch na Jota.
Kutokana na sakata la VAR mwishoni mwa juma lililopita, mabosi wa chama cha waamuzi walikiri kutokea kwa dosari kubwa baada ya Luiz Diaz kunyimwa bao halali dhidi ya Spurs.
Mabosi hao walithibitisha kuwa makosa ya kibinadamu yalichangia makosa kujitokeza katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England, kwani afisa wa VAR alisahau kumwambia refa msaidizi abadili umamuzi wa refa wa kulikataa bao kwa sababu Diaz hakuwa ameotea.