Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klabu zatakiwa kuwa na ofisi rasmi

A7f753cddc09003ac8db83c5c4826b82 Klabu zatakiwa kuwa na ofisi rasmi

Sat, 19 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

VIONGOZI wa klabu za michezo wametakiwa kuandaa mikakati kwa kushirikiana na wadau ili kuwa na ofisi rasmi za kuendesha shughuli zao.

Wito huo umetolewa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Tabia Maulid Mwita, wakati wa ufunguzi wa ofisi ya klabu ya Jang’ombe Boys huko Jang'ombe mlimauni.

Alisema hatua waliyoifanya Boys ni ya kupongezwa na ni ya mfano kwa klabu nyingine.

“Hatua ya klabu kuwa na ofisi ni nzuri na itasaidia kwa kiasi kikubwa kuweza kuendesha shughuli zao kwa ufanisi zaidi,” alisema Tabia.

Pia alisema uamuzi wa klabu hiyo wa kuwa na ofisi ni mzuri na kuwataka waitumie kwa malengo ambayo yamekusudiwa ili kuimarisha viwango vya wachezaji wao.

“Naamini hii ni sehemu nzuri ambayo kila mmoja wenu ameiona na lengo kubwa la kuwa na ofisi hii ni kuweza kufanya majukumu yenu kwa ufanisi ili kuendeleza vipaji vya vijana,” alisema Tabia.

Aliwataka viongozi wa klabu hiyo kuhakikisha wanafanya yale ambayo wamejipangia ili kuhakikisha klabu yao inazidi kuwa juu kimaendeleo.

Mapema katibu wa klabu hiyo, Alawi Haidar Foum alisema jengo la ofisi yao limepatikana kwa jitihada za viongozi wa klabu hiyo pamoja na viongozi wa jimbo lao akiwemo mbunge na mwakilishi ambao wamewasaidia kufikia hapo.

Jang’ombe Boys katika msimu wa 2020/2021 inatarajiwa kushiriki Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja baada ya msimu uliopita kushuka kutoka ligi kuu.

Chanzo: habarileo.co.tz