Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klabu zakumbushwa kukamilisha usajili kabla ya Agosti 31

Tff Office labu zakumbushwa kukamilisha usajili kabla ya Agosti 31

Fri, 25 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezikumbusha Klabu zote za Ligi Kuu ya NBC (NBCPL), Championship League (CL), First League (FL), na Serengeti Women Premier League (SWPL) kufanya usajili na kukamilisha kwa wakati kabla ya kufungwa kwa Dirisha la Usajili Agosti 31, 2023 saa 5:59 usiku.

Kupitia taarifa yake ya leo Agosti 25, 2023 kwa umma TFF imebainisha kuwa mpaka sasa timu zifuatazo hazijafanya usajili wa mchezaji yeyote kwenye mfumo wa usajili wa FIFA Connect:

CHAMPIONSHIP LEAGUE:

1. Transit Camp - Dar es Salaam 2. Copco FC Mwanza

FIRST LEAGUE:

1. TRA FC Kilimanjaro

2. Kurugenzi FC - Simiyu

3. Malimao FC - Katavi

LIGI KUU YA WANAWAKE ya SERENGETI LITE:

1. Geita Gold Queens - Geita

2. Yanga Princess - Dar es Salaam

TFF imeendelea kusisitiza kuwa hakutakuwa na muda wa ziada baada ya kufungwa dirisha la usajili huku ikizikumbusha Klabu zote kukamilisha usajili wa timu za vijana (U20, U17) kwa mujibu wa kanuni ya kila Ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live