Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klabu za Morocco zina kibarua cha kupindua matokeo wikiendi hii

TIMU ZA MOROCCO Klabu za Morocco zina kibarua cha kupindua matokeo wikiendi hii

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwisho wa wiki hii kutakuwa na balaa kubwa nchini Morocco kwa sababu klabu zote tatu (3) za Morocco zilikandwa ugenini kwenye michuano ya CAF sasa zitakuwa nyumbani zikijaribu kupindua matokeo.

Kwenye Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika Wydad Casablanca ilipoteza 1-0 uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar. Raja Casablanca ilikandwa 2-0 na Al Ahly kule Cairo, Misri.

Wawakilishi wa Morocco kwenye Kombe la Shirikisho la CAF ASFAR Club ilikula chuma mbili mbele ya ASM Alger kule nchini Algeria.

MATOKEO YA KLABU ZA MOROCCO baada ya Robo Fainali za kwanza za mashindano ya CAF.

Simba 1-0 Wydad Casablanca [CAF CL] Al Ahly 2-0 Raja Casablanca CAF CL] USM alger 2-0 ASFAR Club [CAF CC]

Chanzo: www.tanzaniaweb.live