Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klabu za Ligi Kuu England zitakavyotesti mitambo pre-season

Capture Arsenal Klabu za Ligi Kuu England zitakavyotesti mitambo pre-season

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ukishindwa kujiandaa, unajiandaa kushindwa. Ndivyo ilivyo.Pre-season ni kitu muhimu kwa kila timu ya mchezo wa soka kwa sababu inatoa nafasi ya timu kujiandaa kwa maana ya kujaribu mifumo yake ya kiuchezaji kabla ya kuanza kwa msimu mpya.

Katika kutambua umuhimu wa kuwa na pre-season baadhi ya klabu za Ligi Kuu England zimeshaweka hadharani ratiba ya mechi zake za kujifua zitakavyokuwa na zitapigwa wapi.

Baada ya kukamilika mikikimikiki ya Euro 2024 na ile ya Copa America, michuano ambayo itakuwa na huduma za baadhi ya mastaa wanaocheza kwenye Ligi Kuu England, basi ratiba rasmi ya timu hizo itaanza kwa maana ya kutafuta namna ya kujifua kabla ya msimu wa 2024-25 kuanza.

Kwa mujibu wa ratiba ya pre-season ya mwaka huu ilivyo, kwa timu za Ligi Kuu England zipo ambazo zitakwenda Marekani huku nyingine zitakwenda kujifua Asia. Katika sehemu mbalimbali kutashuhudiwa mechi za miamba ya Ligi Kuu England zikienda kutesti mitambo kwenye kipindi hiki cha majira ya kiangazi.

Msimu mpya wa Ligi Kuu England unatarajiwa kuanza Agosti 17, hivyo timu zinajaribu kufanya maandalizi ya kuanza kutesti mitambo yao mapema kabla ya mchakamchaka kuanza rasmi.

Arsenal, Aston Villa, Chelsea, Crystal Palace, Liverpool na Man United ni kati ya timu zitakazokwenda kufanya pre-season huko Marekani.

Arsenal

Julai 27 v Man United (SoFi Stadium, LA)

Julai 31 v Liverpool (Lincoln Financial Field, Philadelphia)

Aston Villa

Julai 27 v Columbus Crew (Lower.com Field, Ohio)

Julai 31 v RB Leipzig (Red Bull Arena, New Jersey)

Agosti 3 v Club America (Soldier Field, Chicago)

Agosti 10 v Borussia Dortmund (Signal Iduna Park, Dortmund)

Brighton

Julai 24 v Kashima Antlers (National Stadium, Tokyo)

Julai 28 v Tokyo Verdy, (National Stadium, Tokyo)

Chelsea

Julai 24 v Wrexham (Levi’ Stadium, Santa Clara)

Julai 27 v Celtic (Notre Dame Stadium, Indiana)

Julai 31 v Club America (Mercedes-Benz Stadium, Atlanta)

Agosti 3 v Man City (Ohio Stadium, Columbus)

Agosti 6 v Real Madrid (Bank of America Stadium, Charlotte)

Crystal Palace

Julai 31 v Wolves (Navy-Marine Corps Memorial Stadium, Maryland)

Agosti 3 v West Ham (Raymond James Stadium, Florida)

Fulham

Agosti 10 v Hoffenheim (PreZero Arena, Sinsheim)

Liverpool

Julai 27 v Real Betis (Acrisure Stadium, Pittsburgh)

Julai 31 v Arsenal (Lincoln Financial Field, Philadelphia)

Agosti 3 v Man United (Williams - Brice Stadium, South Carolina)

Man City

Julai 23 v Celtic (Kenan Stadium, Chapel Hill, N.C.)

Julai 27 v AC Milan (Yankee Stadium, New York)

Julai 30 v Barcelona (Camping World Stadium, Orlando)

Agosti 3 v Chelsea (Ohio Stadium, Columbus)

Man United

Julai 15 v Rosenborg (Lerkendal Stadion, Trondheim)

Julai 20 v Rangers (Scottish Gas Murrayfield, Edinburgh)

Julai 27 v Arsenal (SoFi Stadium, LA)

Julai 31 v Real Betis (Snapdragon Stadium, San Diego)

Agosti 3 v Liverpool (Williams - Brice Stadium, South Carolina)

Newcastle United

Julai 31 v Urawa Red Diamonds (Saitama Stadium, Saitama)

Agosti 3 v Yokohama F. Marinos (National Stadium, Tokyo)

Tottenham

Julai 20 v QPR (Loftus Road)

Julai 27 v Vissel Kobe (National Stadium, Tokyo)

West Ham United

Julai 27 v Wolves (EverBank Stadium, Florida)

Agosti 3 v Crystal Palace (Raymond James Stadium, Florida)

Wolves

Julai 27 v West Ham (EverBank Stadium, Florida)

Julai 31 v Crystal Palace (Navy-Marine Corps Memorial Stadium, Maryland)

Chanzo: Mwanaspoti