Klabu AIK Stockholm ya Sweden imewasili nchini usiku huu kwa mwaliko wa Azam FC kwa ajili ya kujenga mahusiano na wenyeji wao hao.
Ugeni huo umeongozwa na mtendaji mkuu wa club hiyo (CEO), Fredrik Söderberg, Mkurugenzi wa Ufundi,(Technical Director)Peter Wennberg, na msaka vipaji mkuu, (Chief Scout)Tobias Ackerman.
Baada ya kuwasili nchini walipokelewa na Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Omary Kuwe, wawakilishi hawa wa klabu hiyo watapata nafasi ya kushuhudia mashindano ya kusaka vipaji yaliyoandaliwa Azam FC.
Timu zaidi ya 10 kutoka akademi mbali mbali za mikoa tofauti hapa nchini zitashiriki, ambazo zina ushirikiano nazo Azam FC kufuatia makubaliano yaliyoingiwa mapema mwezi uliopita.
Mashindano hayo yatashirikisha wachezaji wa chini ya miaka 15, 17 na 20, umri chini ya na chini ya miaka 15 na yataanza Aprili 30 na kumalizika Mei 4.
Dhumuni la ujio huo ni kusimika mahusiano ya klabu hizo mbili katika biashara ya mpira ikiwa ni pamoja na kusaka vipaji katika mashindano hayo.
AIK Stockholm ndiyo klabu iliyomkuza nyota machachari na hatari wa Newcastle United ya England, Alexander Isak.