Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klabu Ligi Kuu zagoma kupunguzwa

6c08c04400a79f2cb79c5a500a43f226 Klabu Ligi Kuu zagoma kupunguzwa

Sat, 17 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KLABU za Ligi Kuu ya England zimegomea Mradi wa Big Picture’, lakini zimekubali hatua ya dharura ya kuzipatia fedha klabu za Ligi Daraja la Pili na Tatu.

Katika mkutano halisi uliofanyika wiki hii, kimsingi klabu zote 20 za Ligi Kuu kwa pamoja zimekubaliana kukataa mapendekezo ya Big Picture, ambayo yangeshuhudia kupungua kwa timu za lligi hiyo kutoka 20 hadi kubaki 18.

MABADILIKO MAKUBWA

Endapo mabadiliko hayo yangekubaliwa, mbali na kupungua kwa idadi ya timu shiriki, pia tungeshuhudia mabadiliko katika utaratibu wote wa upigaji kura wa Ligi Kuu, pamoja na ufadhili katika Ligi ya England na Chama cha Soka (FA).

Klabu hizo pia zimekubaliana kufanya kazi kwa pamoja tena kwa uwazi zaidi katika mpango wowote wa baadae ambao utahusisha muundo au utaratibu wa fedha wa soka la Ungereza.

‘PROJECT BIG PICTURE’?

Wengi wanajiuliza `Project Big Picture’ nini na ina lengo gani? Lengo kubwa la mradi huu ni kuzipunguzia nguvu klabu za Ligi Kuu ya England na kuzisaidia kifedha na Klabu Ligi Kuu zagoma kupunguzwa kuzilinda klabu za madaraja ya chini.

Zikiongozwa na Manchester United na Liverpool na kuungwa mkono na mwenyekiti wa Ligi ya Soka ya Uingereza (EFL) Rick Parry, mipango hiyo ilipendekeza mabadiliko yafuatayo: Kupungua kwa klabu zinazoshiriki Ligi Kuu ya England kutoka 20 hadi kubaki 18 tu, kusiwepo na Kombe la Ligi ya Soka ya England (EFL), kuwepo na hadhi maalumu kwa klabu tisa za muda mrefu zaidi, kama Everton, West Ham na Southampton.

Timu sita tu kati ya tisa ndio zingepewa nafasi ya kupiga kura, endapo kungekuwepo mabadiliko makubwa kama yale ya kiasi cha pauni milioni 250, kama fidia ya haraka kwa EFL.

Klabu zinazoishia katika nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu ya England kubadili nafasi ya sita kwa klabu za Ligi Daraja la Kwanza katika mechi za mchujo zinatakiwa kutoa asilimia 25 ya mapato kwa EFL.

“Zaidi, washirika wa Ligi Kuu wamekubali kufanya kazi pamoja kama klabu 20 ikiwa ni mipango mkakati kwa ajili ya muundo wa baadae wa kulisaidia soka la Uingereza… “Klabu zitafanya kazi kwa kushirikiana, kwa njia ya uwazi, ikilenga kalenda ya mashindano, utawala na uwezo wa kiuendeshaji.

“Mradi huu unaungwa mkono na FA na utahusisha wadau wakiwemo mashabiki, Serikali na bila shaka EFL.” “Soka haliko sawa bila kuwepo mashabiki viwanjani, hivyo hata uchumi wa klabu hautakuwa sawa.

Ligi Kuu na klabu zote bado zina majukumu ya kuhakikisha mashabiki wanarejea salama viwanjani.”

HAKUNA BIFU TENA

Mtend- aji Mkuu wa Ligi Kuu, Richard Masters anakiri kuwa hakuna tatizo baada ya kutoungwa mkono kwa mpango huo, huku akisisitiza kuwa hakuna bifu lolote na EFL.

Masters alielezea kikao cha Jumatano kuwa kilikuwa cha kujenga na chenye manufaa na kukanusha kuwa mapendekezo yoyote yataharibu muonekano wa ligi. “Lakini hatuna bifu na EFL, na sio na klabu.

Tunataka kuwa na uhusiano mzuri nao. Sisi ni washirika wakubwa. “Tuna uhusiano wa kihistoria nao. Hivyo tunataka maendeleo ya kujenga.” Akizungumza na Sky Sports News, Ian Mather – Mtendaji Mkuu wa klabu ya Ligi Daraja la Tatu Cambridge United - alisema: “Itasaidia hizo ni fedha, na tatizo lilikuwa fedha hazikuwepo hapo.

“Nyongeza, Ligi Kuu imeomba mazungumzo zaidi na EFL kuhusu hali halisi ya mapendekezo kutokana na dunia kukumbwa na janga la ugonjwa wa covid-19.”

Chanzo: habarileo.co.tz