Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Klabu 15 za Ligi Kuu zasalimu amri kwa GSM

GSM GROUP LOGO 1 1489x1536.png GSM ameingia mkataba kama mdhamini mwenza Ligi Kuu Bara

Sat, 18 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu 15 kati ya 16 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Bara zimetoka na azimio la kuunga mkono Udhamini wa Kampuni ya GSM kwenye Ligi hiyo na ziko tayari kuvaa nembo za Mdhamini huyo mwenza wa Ligi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi iliyotolewa vilabu hivyo pia vinepongeza juhudi za TFF na Bodi ya Ligi kusaka wadhamini na zimeomba kuendelea na juhudi za kusaka wadhamini wengine.

Kwa taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinadai ni klabu moja tu, ambayo ni Simba SC ndio walioshindwa kuafikiana na suala la kuvaa nembo hiyo.

Hii hapa taarifa ya TFF ikifafanua kwa undani;

Chanzo: www.tanzaniaweb.live