Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizunguzungu Cha European Super League

Arton150017 Kizunguzungu Cha European Super League

Sat, 23 Dec 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Upande upi utashinda? Upande wa European Super League au ule wa Uefa Champions League. Hii ni ligi.

Michuano ya European Super League baada ya kupigwa marufuku sasa imepewa ruhusa ya kufanyika baada ya uamuzi wa mahakama. Sasa vita ni kali dhidi ya Uefa na Fifa.

Manchester United iliyokuwa tayari kucheza awamu ile ya kwanza ya European Super League safari hii, haraka sana imesema hapana. Na sasa, imeripotiwa kuungana na vigogo wengine wa Bundesliga, Bayern Munich kupinga ushiriki kwenye michuano hiyo mipya ya klabu huko Ulaya.

Man United, sambamba na miamba mingine ya Big Six kwenye Ligi Kuu England ilikubaliana na mpango wa kushiriki European Super League awamu ile ya kwanza, Aprili 2021.

Lakini, mashabiki wa timu hizo waliwamo wa Arsenal na Chelsea waliandamana kupinga timu zao kushiriki kwenye michuano hiyo. Hiyo ilisababisha timu hizo za Big Six zilizokuwa miongoni mwa waanzilishi wa mpango huo kujiondoka kwenye michuano hiyo na kuziacha, Real Madrid, Barcelona na Juventus. Hata hivyo, Julai mwaka huu, Juventus ilijitoa kwenye mpango huo na kubaki Barca na Madrid pekee.

Man United ilisema haina mpango wa kujiondoa Uefa. Bayern, ambayo haikuwamo hata kwenye ule mpango wa mwanzo, imepigilia msumali kabisa, ikisema haina mpango wa kuwamo kwenye European Super League.

Klabu nyingine kama Sevilla, AS Roma na Atletico Atletico nazo zimetoa kauli ya kupinga mpango huo. Klabu za Ligi Kuu England, hasa zile za Big Six zimeshafahamu adhabu itakayozikabili endapo kama zitajiunga na michuano hiyo ya Euro-pean Super League. Kinachoelezwa, timu itakayojihusisha na michuano hiyo, kwanza itapigwa faini ya Pauni 25 milioni na itapokonywa pointi, lakini pia inaweza kuondoshwa kwenye Ligi Kuu England.

Jaribio la kwanza la kuanzia michuano hiyo mwaka 2021 lilizihusisha klabu sita kubwa kwenye Ligi Kuu England. Baada ya mashabiki kuandamana, zilijitoa na kubaki kwenye Ligi Kuu England.

Zilipigwa faini, lakini wakati ule kiwango kilikuwa kidogo, hivyo wanafahamu mkwanja utakuwa mrefu endapo kama zitaamua kujiingiza tena kwenye ESL. Mahakama iliambia Uefa na Fifa haina mamlaka kisheria kuzuia michuano hiyo, hivyo ESL ni ruhusa kurudi na kinachofanyika kwa sasa ni kutafuta timu shiriki. Safari hii mambo yamekuwa tofauti. Man United, Liverpool, Arsenal, Chelsea, Manchester City na Tottenham Hotspur, ambazo ni timu kubwa kwenye Ligi Kuu England na zenye mashabiki wengi ambazo zingenogesha michuano hiyo, lakini sasa kuna rungu kali kwelikweli zikijaribu kurudi tena kwenye European Super League.

Klabu ya Ligi Kuu England ikijiingiza kwenye European Super League itakatwa pointi 30. Adhabu kama hiyo ingepata Chelsea au Spurs kwa msimu uliopita zingeshuka daraja, wakati timu nyingine zingekuwa kwenye nafasi za chini kabisa kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Kinachoaminika ni kwamba muswada mpya wa serikali kuhusu soka utaweka kipengele cha kuzuia leseni kwa klabu itakayojiunga na michuano mingine. Kwa maana hiyo, kuna nafasi finyu sana ya Ligi Kuu England itajiunga na European Super League, la kama zitahitaji kutupwa nje kwenye soka la England.

Chanzo: Mwanaspoti