Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizungumkuti Timu ya Taifa ya Equatorial Guinea

Equatorial Guinea Ges (15).jpeg Kizungumkuti Timu ya Taifa ya Equatorial Guinea

Fri, 12 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Equatorial Guinea (Guinea ya Ikweta) inakabiliwa na mkwamo katika mazungumzo na serikali, huku wachezaji wakiongozwa na nahodha Emilio Nsue wakidai Euro 16,000 kila mmoja kama bonasi ya kufuzu kwa #AFCON2023 na Euro 6,000 kwa kila mechi huko Ivory Coast, bila kujali matokeo.

Haya yamefichuliwa wakati wa mkutano katika Hazina Kuu ya Serikali, ambapo wachezaji walielezwa kuhusu makadirio ya kiuchumi ya serikali kwa ushiriki wao katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa.

Awali wachezaji hao walikuwa wameomba Euro 3000 kwa kila mechi, mahitaji ambayo yalitimizwa baada ya mazungumzo na Shirikisho la Soka na Wizara ya Michezo lakini kuna mabadiliko ya mawazo, na hivyo, madai yao yameongezeka.

Hali bado si shwari wakati mazungumzo yakiendelea huku kukiwa na hali ya sintofahamu kabla ya mchezo wao wa kwanza wa AFCON dhidi ya Nigeria siku ya Jumapili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live