Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Kizuguto aula AFL

Kizuguto Kk Baraka Kizuguto

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Maofisa wawili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Baraka Kizuguto na Clifford Ndimbo wameteuliwa kusimamia idara tofauti katika mechi ya uzinduzi wa mashindano ya African Football League (AFL) kati ya Simba na Al Ahly, Ijumaa hii katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salam.

Baraka Kizuguto ameteuliwa kuwa Meneja wa Kituo cha mchezo huo, nafasi ambayo inatumika kwa mara ya kwanza katika medani ya soka barani Afrika.

Nafasi hiyo ambayo Kizuguto atakuwa wa kwanza barani Afrika kuitumikia, majukumu yake makubwa ni kusimamia shughuli zote zinazohusu mchezo kwa kushirikiana na idara nyingine.

Baadhi ya shughuli hizo ni usimamizi wa mahitaji muhimu ya mchezo, usimamizi wa matukio ya mechi, usimamizi wa timu iliyo ugenini na usimamizi wa eneo la kuchezea.

Kwa upande wa Ndimbo, yeye atakuwa na jukumu moja kuu la kusimamia masuala yote yahusuyo habari kabla, wakati na baada ya tukio hilo pamoja na usimamizi wa wanahabari watakaoripoti uzinduzi huo.

Huu ni muendelezo wa Ndimbo na Kizuguto kuteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf), kusimamia michezo ya kimataifa ndani na nje ya Tanzania.

Wakati Ndimbo akiteuliwa mara kwa mara kusimamia masuala ya habari, Kizuguto yeye alikuwa akiteuliwa kuhudumu nafasi ya mratibu wa mchezo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live